Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Pwani Prof Halimu Shauri. [Picha: Halimu Shauri/ twitter.com]
Baadhi ya wasomi eneo la Pwani wamepinga hatua ya wanasiasa ya kutaka eneo hilo kujitenga.Wasomi hao wamesema kuwa hatua hiyo haifai kuchukuliwa kwa kuwa itawatenganisha Wakenya.Wakiongozwa na mhadhiri wa Chuo kikuu cha Pwani Prof Halimu Shauri, wasomi hao walisema kuwa viongozi wa kisiasa wanapaswa kuimarisha miundo misingi na kuleta maendeleo badala ya kutaka eneo hilo kujitenga.Prof Shauri alisema kuwa jamii ya Pwani inapaswa kupewa elimu ili kufahamu ni vipi miundo misingi itakavyoboreshwa badala ya msukumo wa kutaka kujitenga.“Wananchi wanataka maendeleo wala sio kusisitiza msukumo wa Pwani kujitenga ambao hauna manufaa kwa mpwani mlala hoi,” alisema Prof Shauri.Akizungumza na wanahabari siku ya Jumapili, Shauri alisema kuwa elimu ni njia moja wapo ya kukabiliana na ukosefu wa maendeleo katika kanda nzima ya Pwani, wala sio kujitenga kwa eneo hilo.Shauri alisema kuwa viongozi wa kisiasa wanapaswa kuwa na msukumo mkubwa wa kuhakikisha kuwa eneo la Pwani limepata miradi kutoka kwa serikali kuu ambayo itaboresha maisha ya wakaazi.“Wanasiasa wanafaa kuhakikisha wakaazi wa Pwani wanapata haki sawa za maendeleo kutoka kwa serikali kuu wala sio kutaka kuwatenganisha Wapwani na taifa la Kenya,” alisema Shauri.Amewataka wanasiasa kuwekeza vyema kwenye elimu na kuwadhamini wanafunzi werevu kutoka jamii maskini ili waweze kujiunga na vyuo vikuu.“Iwapo wanasiasa watawekeza vyema kwa miradi mbali mbali yenye manufaa, basi Wapwani watakuwa na maisha bora zaidi,” alisema Shauri.Kauli hii inajiri baada ya baadhi ya viongozi wa Pwani akiwemo Gavana wa Mombasa Hassan Joho na mwenzake wa Kilifi Amason King kushikilia kuwa bado azma yao ya Pwani kujitenga ingalipo na mikakati bado inaendelea.Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by joining this group and have it published. http://bit.ly/2BipYa6