Wataalamu katika sekta ya afya kaunti ya Nakuru wametaka kubuniwa kwa sheria na sera zitakazoweza kusaidia kukumbana na magonjwa yasiyo ambukizwa maarufu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Haya yamejiri huku wataalamu hao wakisema kuwa magonjwa hayo yamekuwa yakiongezeka kila siku katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa maswala ya afya katika kaunti hiyo Dkt Joseph Leani, sheria hizo zitawezesha kukabiliana na magonjwa hayo na pia itawezesha washika dau katika sekta hiyo kushirikiana kwa pamoja ili kukumbana na maswala hayo.

"Upungufu wa wauguzi eneo hili unaadhiri pakubwa huduma zinazotolewa huswa kwenye zahanati za kaunti hii." Bw Lenai alikariri.

Akizungumza Jumatatu baada ya kuzuru hospitali kuu ya wilaya ya Naivasha, mkuu huyo pia ameitaka bunge la kaunti hiyo kupitisha sheria ya rasilimali za kiafya ili wauguzi zaidi waweze kuajiriwa.