Afisa mkuu mtendaji katika Benki ya Equity tawi la Eldoret katika Kaunti ya Uasin Gishu wamekusanyika mjini Eldoret leo hii na wanafunzi waliofanya vyema katika mtihani wao wa kidato cha nne mwaka jana na kutuzwa katika mradi wa ‘Wings to Fly’.

Share news tips with us here at Hivisasa

Afisa Joseph Muiruri alisema kwamba mradi huo unapania kuwafaidi zaidi ya wanafunzi 20 kutoka familia zisizojiweza kifedha katika Kaunti ya Uasin Gishu waliopata alama ya A- (hasi) na A.

Kati ya walionufaika na mradi huo ni pamoja na Elijah Letio aliyekua mwanafunzi katika Shule ya Upili ya Lodwar katika Kaunti ya Turkana ambaye alikua na alama ya A (84), Faith Ng’eno aliyekuwa na alama ya A (83) alikua mwanafunzi katika Shule ya Upili ya Loreto Matunda katika Kaunti ya Uasin Gishu miongoni mwa wengine 18.

Akizungumza na Waandishi wa habari mjini Eldoret, Muiruri alisema kuwa wale waliopata alama hizo watajiunga na Vyuo Vikuu vya kimataifa na zaidi ya wanafunzi 2,023 wamenufaika na mradi huo.

Naibu Gavana katika Kaunti ya Uasin Gishu Daniel Chemno aliyasihi mashirika mengine kuiga mfano wa Benki hiyo ili kuwasaidia wanafunzi wengi katika jamii.

Chemno aliongeza kuwa kati ya walionufaika, 11 kati yao ni wale waliofadhiliwa kujiunga na Shule za Upili miaka minne zilizopita.

Chemno aliwaomba walionufaika na ufadhili huo kuwasaidia vile vile na wengine katika jamii.