Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Evans Achoki katika hafla ya awali. [Picha/ the-star.co.ke]

Share news tips with us here at Hivisasa

Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Evans Achoki amewahakikishia usalama wa kutosha wapiga kura watakaoshiriki marudio ya uchaguzi ya urais tarehe Oktoba 26.Achoki amedokeza kuwa mikakati kabambe ya kulinda wapiga kura imewekwa na kuwataka Wakaazi wa Mombasa kutokuwa na hofu.Akizungumza katika uwanja wa Tononoka wakati wa sherehe za Mashujaa siku ya Ijumaa, Achoki aliwataka wakaazi kujitokeza kwa wingi na kushiriki uchaguzi huo.“Jitokezeni kwa wingi mupige kura kwani usalama umeimarishwa hapa Mombasa,” alisema Achoki.Achoko amesisitiza kuwa watakaojaribu kuvuruga uchaguzi huo watakabiliwa kisheria.“Hatutakubali watu kuvuruga uchaguzi. Watakao zua fujo watakabiliwa vilivyo,” alisema Achoki.Achoki alisema kuwa kushiriki uchaguzi ni haki ya kikatiba ya kila Mkenya na yeyote ambaye hataki kushiriki sharti abaki nyumbani badala ya kutaka kuzuia wengine kushiriki kwenye zoezi hilo.Aidha, ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na maafisa wa polisi kwa kutoa taarifa kuhusiana na yeyote anayepanga kutatiza shughuli hiyo ya uchaguzi.