Vijana watano wenye umri wa makamo wamehukumiwa kifo na mahakama moja mjini Mombasa kwa kosa la wizi wa mabavu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Watano hao, Peter Warui Kamau, Mustafa Ali Mwambeyu, Vincent Okoth Matinde, Basilio Micheal na Derrick Kariuki Kamau walipatikana na makosa ya kutekeleza wizi huo wa mnamo Oktoba 15 mwaka 2013.

Koti ilibaini kuwa watano hao wakiwa wamejihami kwa visu, bunduki, na mapanga walimvamia Sydney Anthony na kutekeleza wizi wa mali ya thamani ya shilingi elfu 42 eneo la Nyali.

Hakimu Irene Ruguru katika hukumu yake aliwapa adhabu ya kifo na kudokeza kuwa hilo lingekuwa funzo kwao na wengine wenye nia kama hiyo.

“Hii itakuwa funzo kwa wengine wanaotaka kutekeleza wizi nchini,” alisema Ruguru.

Hata hivyo, mahakama hiyo imewapa watano hao muda wa siku 14 kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.