Watu watatu wameshtakiwa katika Mahakama ya Mombasa kwa madai ya ulaghai.
Washtakiwa hao, Moses Njuguna, Eunice Nyambura na Dickson Kimani wanadaiwa kumlaghai Murithi Rungu.
Inadaiwa kuwa washtakiwa hao walimdanganya mlalamishi kuwa wangeuza gunia 200 za mchele zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne kwenye duka la jumla la Tuskys, mjini Mombasa.
Washukiwa hao walikana madai hayo mbele ya Hakimu Irene Ruguru siku ya Ijumaa.
Hakimu Ruguru aliagiza washukiwa hao kutoachiliwa kwa dhamana baada ya upande wa mashtaka kusema wanakabiliwa na kesi nyingine katika Mahakama ya Mombasa.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe 6 mwezi Juni.