Mahakama ya Mombasa. Hakimu Francis Kyiambia aliwaachilia washukiwa hao kwa dhamana ya shilingi milioni moja. Picha: Haramo Ali/ hivisasa.com
Washukiwa watatu wanaokabiliwa na shtaka la wizi wa fedha za kampuni ya marehemu Tahir Sheikh Said (TSS) wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa.
Watatu hao, Aweys Mohamed, Zein Mohammed Ahmed na Zahir Gulam Hussei Khaku wanadaiwa kugushi cheti cha kampuni ya TSS na kufanikiwa kujipatia zaidi ya shilingi bilioni moja.Washukiwa hao hata hivyo wamekanusha mashtaka hayo mbele ya Mahakama ya Mombasa.Wakili wao, Cliff Ombeta, aliiomba mahakama kuwaachilia wateja wake kwa dhamana kwa kuwa ni haki yao ya kikatiba.Hakimu Francis Kyiambia alikubali ombi hilo na kuachilia washukiwa hao kwa dhamana ya shilingi milioni moja.Uchunguzi zaidi unafanywa ili kugundua benki ambazo zilihusika katika kutekeleza kashfa hiyo.