Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Vijana watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la wizi wa mabavu.

Washukiwa hao, Mohammed Abumau, Kelvin Mwachii na Farah Hussein wanadaiwa kumuibia Janet Auma pochi alipokuwa akitoka katika benki mmoja mjini Mombasa.

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama kuwa vijana hao wanadaiwa kuwa walikuwa wamejihami kwa silaha na kutishia kumua mlalamishi huyo.

Watatu hao walikana mashtaka dhidi yao mbele ya Hakimu Teresia Matheka siku ya Alhamisi.

Hakimu Matheka aliagiza vijana hao kuachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja kila mmoja.