Watu watatu wameshtakiwa katika Mahakama ya Mombasa kwa madai ya wizi.
Washukiwa hao, Athumani Kamau, Benjamin Amoche na Elizabeth Mwikali wanadaiwa kuiba shilingi laki moja pesa taslimu, mnamo tarehe 26 mwezi Januari, katika eneo la Shimanzi jijini Mombasa.
Washukiwa hao walikana mashtaka hayo mbele ya Hakimu Diana Mochache siku ya Jumanne.
Hakimu Mochache aliagiza washukiwa hao kuachiiwa kwa dhamana ya shilingi laki mbili kila mmoja.
Aidha, hakimu huyo aliamuru washukiwa hao kupelekwa katika hospitali ya serkali kubaini hali yao ya kiafya baada ya wakili wao kudai wateja wake walipigwa na maafisa wa usalama na kuwasababishia madhara.
Kesi hiyo itatajwa siku ya Alhamisi.