Wapandaji miche [green town] katika kaunti ya Kisii wameiomba serikali ya kaunti hiyo kuwasaidia ili kukuza biashara zao.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakiongea katika shamba lao  lililoko karibu na Daraja Mbili hii leo wamesema biashara zao zimerudi chini na wamekadhiria hasara  kubwa kutokana na kiangazi kutoka mwezi wa disemba mwaka jana.

Aidha, wameiomba serikali hiyo kuwanunulia mbegu za miti ya kisasa ilikuendeleza  upanzi wao.Wameelezea kuwa mbegu hizo uuzwa kwa bei ghali,pesa ambazo hawawezi kuwa nazo.

“Tunaomba serikali kutukumbuka na kutusaidia kupata mbegu za kisasa na kututafutilia soko ambalo tutaweza uza miche zetu kwa bei ya juu ili kupata faida na kuongeza kiwango cha upanzi wetu,”alisema mwenyekiti Joseph Omete.

Aliongezea kuwa chama chao cha upanzi kuna wanachama 27, ambao kwa sasa wanataka kujiadikisha ili kunufaika na pesa za Uwezo Fund.

Kulingana na katibu wao  Marcalius Samson soko lao limekosekana kutokana na mawakala [brockers] ambao ununua miche kwa bei ya chini na kuenda kuuza kwa bei ya juu bila kuwajali wapanzi hao.

“kuna sherehe nyingi zinazofanyika katika kaunti na zinaitaji upanzi wa miti ambayo tuko nayo ,lakini hakuna mwenye amewai nunua kutoka kwetu ili nazi tunufaike wakati watakaponunua kutoka kwetu,”alieezea  Samson.

Kwingineko wameiomba sekta ya mazingira kuwachukulia hatua kali wanaochoma taili za gari  karibu na shamba lao ambao huchangia kukauka kwa miche yao.Taili hizo zinachomwa na wanaotengeneza magari karibu na shamba lao kitu wanaofya afya yao kwa kuwa hata moshi huwasumbua na wataeza patwa na magonjwa mbalimbali. Wapanzi hao wamepongeza shirika linalosimamia mazingira [ NEMA] kwa kuwatetea kila mara  wakati shamba lao linatakunyakuliwa na watu fulani .

“shirika hilo limekuwa la mswaada kuu kwetu kwa kuwa shamba letu huwa linataka kunyakuliwa na baadhi ya wale walio na pesa   katika kaunti hii” alisema Joseph Ondieki  mwekahasina .

Wapanzi hao wamefanya kazi yao  ya upanzi kwa takribani miaka kumi bila kilio chao kusikizwa na kupata matunda mema.