Huku benki ya Chase tawi la Nakuru ikifunguliwa, wakaazi wa Nakuru sasa wameihimiza serikali kuhakikisha kuwa fedha za wateja wa benki hiyo zinausalama wa kutosha kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa ndan wa taasisi za kifedha.
Mteja mmoja, Joseph Ngugi Gitau ambaye aliye na akaunti mbili kwenye benki hiyo moja ya kampuni yake na nyingine ikiwa ya makaazi ya nyumba ya watoto alisema; ‘ Serikali iangalie benki zetu. Kama benki inaonekana sio nzuri, hakuna haja ya kuiwacha. Ni vyema iondoke,’ alisema Gitau.
Ingawa alikiri kuwa walipokea huduma nzuri kabla benki hiyo ifungwe, alikariri kuwa wanahofia kuhusiana na uongozi wa benki hiyo.
‘ Kabla Chase Bank ifungwe tulikuwa tunapata huduma nzuri. Lakini kwa sasa tunahofu, hatujui huduma zitakuwa vipi pamoja na wasimamizi wake,’ aliongeza Gitau.
Kwa upande wake, Josphat Chege ambaye ni mfanyibiashara mjini Nakuru alisema serikali inafaa kuhakikisha kuwa wakurugenzi wa benki hawapati mikopo ya benki katika benki ambazo wanafanyakazi.
Ameongeza kuwa iwapo watachukua mikopo, mikopo hiyo inafaa kuchukuliwa kama mikipo yoyote ile ambayo imechukuliwa na wateja wa benki .
Ameeleza kuwa amefanikiwa kuhamisha kiwango kadogo cha fedha zake kutoka kwa benki hiyo hadi kwa benki nyingine na anatumia kuwa iwapo imani ya wakenya itarejeshwa kuhusiana na benki ya Chase, basi atarejesha fedha zake kwenye benki hiyo.
‘ Nimetoa kiwango kadogo cha fedha kwenye kaunti yangu ya Chase bank kwa benki nyingine lakini baada ya mambo kuwa shwari na imani ya wakenya kurejea kwenye benki hii, nitarejesha fedha zangu zote kwenye kaunti ,’ alisema Chege.
Hata hivyo, baada ya benki hizo kufunguliwa, juhudi za waandishi wa habari za kutaka kuzungumza na maafisa wa benki hiyo kuhusiana na maswala hayo ziliambulia patupu baada yao kuwaagiza kuelekeza maswali yao katika makao makuu ya benki hiyo ili waweze kupata taarifa rasmi.