Share news tips with us here at Hivisasa

Wateja wa Benki ya Imperial iliyofungwa mwaka uliopita kutokana na ukosefu wa fedha wamefika katika Mahakama ya Mombasa wakitaka mahakama hiyo iamuru Benki Kuu ya Kenya kuwapa fedha zao walizokuwa wamehifadhi katika benki hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari katika majengo ya mahakama siku ya Jumanne, wakili wa wateja hao, Francis Kadima, alisema kuwa kuzuiliwa kwa fedha ya wateja wake kumeathiri biashara yao, hali iliyosababisha maisha yao kubadilika.

Kadima alisema kuwa baadhi ya wateja wake wanalazimika kuishi maisha ya umaskini ilhali wana mabilioni ya pesa kwenye benki.

“Wateja hawapaswi kuadhibiwa kwa kuweka pesa zao kwenye benki. Kama benki ilikuwa na makosa, inafaa iadhibiwe na wala sio wateja,” alisema Kadima.