Dr Khadija Shikeli the director of health in Mombasa county. [Picha/barakafm.org]
Wagonjwa 5 kati ya 17 na saba waliokuwa wanaharisha na kutapika wamebainika kuwa na ugonjwa wa kipindupindu katika eneo bunge la Likoni kaunti ya Mombasa.
Akitoa taarifa hiyo mkurugenzi mkuu wa afya kaunti ya Mombasa daktar Khadija Shikeli, amesema kuwa watu 4 wamefariki katika eneo hilo kati ya tarehe 30 Disemba hadi 2 Januari ya mwaka huu katika gatuzi dogo la Likoni.
Akizungumza na wanahabri siku ya Ijumaa,alisema kuwa watu wawili walifariki na kipindupindu kutoka mtaa wa Maka Majengo Mapya,huku wengine wawili kutoka mtaa wa Vyemani huko Shikaadabu.
“Jumla ya watu wanne walifariki katika eneo bunge hilo la Likoni kwa sasa”,alisema Shikeli.
Kutokana na hilo idara ya afya imetoa tahadhari kwa wakaazi wa Mombasa kutilia mkazo swala la usafi ili kuepuka maambukizi zaidi.
Wakati huo huo idara hiyo imeanzisha tena shughuli za kuzuia uuzaji wa vyakula kiholela huku ilani ikitolewa kwa wale wote wasio na vibali vya afya vya kuendesha biashara zao.
Itakumbukwa kuwa mapema mwezi Disemba idara hiyo ilifunga vibanda vyote vya vyakula pamoja na wauzaji wa maji wasio na vibali hivyo baada ya mkurupuko huo kushudiwa kuenea kwa kasi hasa katika maeneo ya Jomvo na Changamwe.
Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by Joining this group, and have it published. https://chat.whatsapp.com/5K1mGBnRVB46Mixhdh5caF