Watu wane walifariki kwenye ajali ya barabarani katika eneo la St Mary’s barabara kuu ya Nakuru-Nairobi Jumanne jioni.
Wanne hao walifariki baada ya matatu moja ya kampuni ya North Rift Kugongana ana kwa ana na basi.
Walioshuhudia kisa hicho wanasema kuwa matatu hiyo ilikuwa ikiendeshwa kwa kasi.
“Matatu ilikuwa inatoka Nairobi wakati ambapo ilikuwa ikiendeshwa kwa kasi. Ilijaribu kupita gari nyingine na ndipo ikakutana na basin a kugongana ana kwa ana,” Peter Nderitu Muthee alisema.
Aidha abiria wengine kadhaa walijeruhiwa kwenye kisa hicho na kukimbizwa hospitalini.
OCPD wa Gilgil Serah Koki alidhibitisha ajali hiyo na kuwataka madereva kuwa makini.