Wanamgambo wa al-Shabaab wakifanya mazoezi hapo awali. [Photo/ pinterest.com]
Watu wanne wanaripotiwa kuuawa na washukiwa wa kundi la al-Shabaab usiku wa kuamkia siku ya Jumatano katika kijiji cha Bobo, Wadi ya Hindi, Kaunti ya Lamu.Kulingana na mkaazi ambaye hakutaka kutajwa, wanne hao waliuaawa kwa kupigwa risasi wakiwa majumbani mwao baada ya watu wanaodaiwa kuwa wanamgambo wa kundi la al-shabaab kushambulia kijiji hicho.Mauaji hayo yanajiri siku moja tu baada ya mtu mmoja kutekwa nyara siku ya Jumanne na wanamgambo hao.Wakaazi wa eneo hilo walifanya maandamo siku ya Jumatano katika barabara ya Mombasa-Lamu kulalamikia ukosefu wa usalama.Wakaazi hao wamewakosoa maafisa wa usalama kwa kuchelewa kufika katika eneo hilo baada ya shambulizi hilo.Akizungumzia tukio hilo, Kamishna wa Kaunti ya Lamu Gilbert Kitiyo alisema kuwa maafisa wakuu wa usalama wameandaa mkutano na watatoa maelezo zaidi baada ya kujadiliana.Wiki moja iliyopita mshirikishi mkuu wa ukanda ya Pwani Nelson Marwa alitangaza kuwa maafisa wa KDF watalipua msitu wa Boni, ambao unadaiwa kuwa maficho ya wanamgambo hao kama njia moja ya kukabiliana na ugaidi nchini.