Wanafunzi wanne wa Shule ya msingi ya Kisauni pamoja na watu wengine watatu walipoteza maisha yao baada ya kuhusika katika ajali kwenye barabara ya Mombasa-Lungalunga, eneo la Kanana, Kaunti ya Kwale.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wanafunzi hao walikuwa wanarejea nyumbani katika matatu ya kukodisha baada ya kuhudhuria hafla ya kuzuru mapango ya Shimoni.

Akithibitisha kisa hicho, Mkuu wa polisi wa eneo la Shimoni Abdullah Tato alisema kuwa bali na wanafunzi hao, mama mmoja na watoto wake wawili waliokuwa wakisubiri kuabiri gari pia waliangamia katika ajali hiyo.

Tato alisema kuwa ajali hiyo inakisiwa kuwa ilisababishwa na dereva wa matatu hiyo aliyejaribu kuingia makutano ya barabara ya Kanana, huku kukiwa na gari nyingine iliyokuwa ikitokea Mombasa.

Matatu hiyo iligongana na lori lililokuwa likiendesha kwa kasi kuelekea mpakani wa Kenya na Tanzania.