Watu watatu wameaga dunia baada ya kuhusika kwenye ajali ya barabara katika eneo la Changamwe.
Inaripotiwa kuwa watatu hao, akiwemo mtoto mmoja, walifariki papo hapo baada ya kungonwa na gari aina la pickup.
Akithibitisha kisa hicho cha Jumatatu, mkuu wa polisi eneo la Changamwe Joseph Muthee, alisema kuwa dereva wa gari hilo alishindwa kulidhibiti na kuwagonga wapita njia hao.
Watu wengine wanne waliripotiwa kujeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea mwendo wa 7.30 usiku.
Wanne hao wanaendelea kupokea matibabu katika Hospitali ya Makadara.
Bwana Muthee alisema kuwa maafisa wa polisi wameanzisha uchunguzi kubaini kilichosababisha ajali hiyo.