Watu wawili wamelazwa kwenye hospitali ya Naivasha baada ya mshambulizi kwaenye mzozo wa shamba la Utheri wa Lari Naivasha. Wawili hao wanadaiwa kushambuliwa na kundi la wafugaji ambalo linadai umiliki wa shamba hilo.
“Kundi la vijana wa wamaasai liliwashambulia wazee hao wawili na kuwaumiza vibaya. Kumekuwa na mzozo kati ya jamii hizi mbili kuhusu ni nani mmiliki halisi wa shamba hilo,” mkaazi ambaye hakutaka kutajwa alisema.
Mbunge wa Nakuru Kimani Ngunjiri aliwaongoza wabunge kadhaa Jumatano kuzuru wawili hao huku wakitaka mzozo uliopo kukabiliwa. Ngunjiri aliahidi kufanya mkutano na viongozi kutoka Kajiado, Narok na Nakuru ili kumaliza mzozo huo.
Daktari kwenye hospitali hiyo alisema wawili hao walikuwa na majeraha ya kukatwa lakini wanapata nafuu.