Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa Nakuru Magharibi Samwel Arama amekanusha madai kwamba baadhi ya wakaazi wa Nakuru wamekuwa wakifaidika na fedha za hazina ya maeneo bunge CDF kutoka kwa maeneo bunge ya Nakuru Magharibi na Nakuru Mashariki kwa upande mmoja.

Akitaja taarifa hizo kama uvumi, mbunge huyo alikariri kwamba kuna mikakati inayofuatwa mtu anapotaka kupata fedha inayomwezesha kupata fedha hizo.

Kwenye mahojiano na wandishi huyu Jumatatu, Mbunge huyo aidha amesema kuna stakabadhi kadhaa zinzohitajika mtu anapoomba fedha hizo za hazina ya maeneo bunge CDF akisema ni kutokana na stakabadhi hizo ambapo mtu hupata fedha hizo.

Pamoja na hayo, aliashiria kwamba kuna taratibu zinazofwata katika kuhakikisha kwamba hundi zinazoandikwa kutokana na wanaofaidi kutokana na mradi huo zinafikia taasisi husika na wala sio watu binafsi.

Ni hundi ambazo alisema huandamana na stakabadhi za mhusika kama vile kadi yake ya kuhakikisha kwamba yeye ni mpiga kura aliyesajiliwa katika eneo bunge husika.

Matamshi ya Mbunge huyu yanajiri huku madai yakiibuka kwamba kuna baadhi ya watu ambao wamebuni njia za kuweza kujifaidia kutokana na fedha za hazina ya CDF kutoka kwa maeneo bunge mawili.