Kamishna wa kaunti ya Mombasa Mohamed Maalim ameitaka halmashauri ya kukabiliana na utumizi wa mihadarati nchini NACADA kujitahidi kuwasilisha huduma zake katika kaunti hiyo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Maalim ameeleza kusikitishwa kwake na ongezeko la idadi ya waathiriwa wa mihadarati, akisema wengi hawana uwezo wa kujiunga na vituo vya kurekebisha tabia vya kibinafsi kutokana na gharama ya juu ya malipo. 

Akizungumza na wanahabari afisini mwake, afisa huyo amelitaka shirika hilo kujizatiti kuhakikisha waathiriwa wa mihadarati katika kaunti hii wananufaika na huduma za shirika hilo. 

Wakati huo huo, amewaonya walanguzi wa mihadarati dhidi ya kuendeleza shughuli zao katika kaunti hiyo.