Katibu wa muungano wa wauguzi tawi la Mombasa Peter Maroko. [PHOTO/mediamaxnetwork.co.ke]
Wauguzi kaunti ya Mombasa wametishia kugoma upya jumatatu wiki ijayo kudai mishahara ya miezi sita.
Katibu wa muungano wa wauguzi tawi la Mombasa Peter Maroko amesema kuwa wauguzi hao hawajalipwa mishahara ya kuanzia mwezi Juni.
“Hatujalipwa kuanzia mwezi Juni,huu ni unyanyasaji mkubwaa”,alisema Maroko.
Akizungumza kwenye kikao na wanahabari siku ya Jumanne,anadi serikali ya kaunti ya Mombasa imekuwa ikiwapa ahadi za uongo na kukosa kuafikia mkataba wa kitaifa uliotiwa sahihi baina ya serikali za kaunti na ile ya kitaifa.
“Tumechoka kupewa ahadi za uongo nah ii serikali ya Mombasa,hawatimizi ahadi zao”,alisema Maroko.
Maroko alisema kuwa wanapitia maisha magumu kwa kukosa pesa za kukimu mahitaji yao ya kifamilia.
“Tunapitia changamoto za maisha,hatuna pesa za kuwakidhi mahitaji ya familia zetu”,alisema Maroko.