Huku wakristo wakiendelea kusherekea siku kuu ya Pasaka kote ulimwenguni, waumini wa kanisani Katoliki eneo la Mtopanga wamehimizwa kuwa na ushirikiano na kuwasaidia wasiojiweza.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiwahubiria waumini wa kanisa Katoliki la Mtakatifu Yakobo eneo la Mtopanga mjini Mombasa siku ya Jumatatu katika Ibada ya Pasaka, Padri wa Kanisa hilo Aumogast Mudawida amesema kuwa waumini wanafaa kutafakari mateso aliyopitia Yesu Kristu na kutangamana katika kuwasaidia wasiojiweza.

Amesema kuwa lazima kwa jamii ya Mombasa kushirikiana katika kila jambo ili kuona kuwa wakenya wanaishi kwa amani na kila mkristu na mkenya kwa jumla ana jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa taifa hili lina amani na uiano.

“Ni Jukumu la kila mkristu na mkenya kwa jumla kuhakikisha kuwa mnashirikiana na kuwasiadia wasiojiweza ili kuona kuwa taifa hili linadumisha Amani,” alisema Mudawida.

Wakati huo huo amepongeza juhudi za maafisa wa polisi kuhakikisha kuwa usalama wa kaunti nzima ya Mombasa unahimarishwa hasa wakati huu wa shamra shamra za pasaka.