Waumini wa kanisa la Kipentekoste wameunga mkono msimamo wa muungano wa makanisa nchini wa kumtaka mwanasheria mkuu Githu Muigai kujiuzulu kwa kushindwa kuishauri serikali ipasavyo kuhusu masuala ya kidini.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakiongozwa na Joesph Kazungu, waumini hao walisema kuwa waliamua kuchukua msimamo huo kufuatia kusajiliwa kwa kikundi cha wasioamini uwepo wa Mungu hapa nchini.

Wakizungumza na mwandishi huyu, waumini hao walisema kuwa wanaunga mkono shinikizo za muungano huo kutaka sajili ya kundi hilo kufutiliwa mbali kwa msingi kwamba linaenda kinyume na katiba inayotambua kuwepo kwa Mungu pamoja na kuipa nchi sura mbaya.

Kazungu alidai kuwa kundi hilo limepotosha wengine na halifai kutopewa nafasi kabisa.

Aidha, alisema kuwa muungano huo wenye makao yake makuu jijini Nairobi, unaunga mkono kauli ya Askofu Stephen Ndicho aliyesema kuwa huenda wakafika mahakamani kutaka kutupiliwa mbali kwa kundi hilo.