Wamiliki wa maduka ya kuuza dawa kinyume cha sheria wamehukumia kifungo cha miezi 6 gerezani kila mmoja.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Siku ya Alhamisi upande wa mashtaka uliambia mahakama kuwa, Debra Mueni, Chepelesi Ateka na Baraza Hores wanadaiwa kujihusha na biashara hiyo pasi kuwa na vibali eneo la Chaani huko Changamwe na eneo la uwanja wa Makadara jijini Mombasa kati ya Aprili 11, 2016 na Aprili 13, 2016.

Wote wamekubali mashtaka hayo mbele ya hakimu katika mahakama ya Mombasa, Diana Mochache.

Debra ameachiliwa kwa faini ya shilingi 60,000 ama kutumikia kifungo cha miezi 6 gerezani, huku Chepelesi akitozwa faini ya shilingi 65,000 ama kifungo cha miezi 6 jela.