Wauzaji wa miwa katika mji wa kisii wameombwa kudumisha usafi katika mji huo au kutoruhusiwa kufanya biashara katikati ya mji huo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea hii leo katika mji wa Kisii mwenyekiti wa kundi linalofanya usafi katika mji wa kisii na viunga vyake (Minto Muungano youth Group), Kepha King’oina, alisema kuwa wengi wa wauzaaji hao hawazinagatii usafi.

 Alisema kuwa wauzaju haonhutupa magada ya miwa mahali popote nakufanya mji huo kuwa na uchafu mwingi.

“Wauzaji wa miwa katika mji wa Kisii wamekuwa wakichafua mji huu bila kujali wale wanaofanya kazi ya kufagia na kusafisha mji huu,” alisema Kepha.

Kepha amewaomba wote wanao uza miwa katikati ya mji wa Kisii kuwajibika na kuhakikisha kuwa mji huo unaendelea kuwa msafi bila kutupa magada yao mahali popote.

Aidha amewaomba wazazi wale wanaowatuma wanao kufanya biashara hizo kuwafunza watoto hao umuhimu wa mazingirea safi na jinsi wanastahili kulinda mazingira yao.

Kwingineko Kepha ameomba serikali ya kaunti kutoa watoto wanao randaranda mitaani ambao wameonekana kurundi na kuwapeleka  katika makazi ya watoto mayatima.

Watoto hao kwa sasa  wanachangia pakubwa kuongeza kwa uchafu katika mji huo kwa kua huenda chooni mahali popote kitu ambacho kinawakere wafanyikazi  wa kufagia.