Serikali kuu imehimizwa kuondoa marufuku ya kutotoka nje nyakati za usiku kwa wakaazi wa Kiunga, Faza na Kizingitini ili wakaazi hao waendelea na shughuli zao za uvuvi bila vizuizi.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Naibu mwenyekiti wa Shirika la Save Lamu katika kaunti ya Lamu Mohamed Mbwana amesema kuwa ni lazima serikali kuondoa marufuku hiyo kwani kaunti ya Lamu iko salama ili swala la uimarishaji uchumi kutekelezwa kikamilifu.

Kwenye mkao na wanahabari mjini Mombasa siku ya Alhamisi, Mbwana alisema kuwa serikali iko na njama ya kuangamiza uchumi wa kaunti ya Lamu kutokana na kukandamiza kitega uchumi cha eneo hilo hasa uvuvi wa samaki kwani serikali imekosa kuangazia swala hilo.

"Tunataka serikali kutufikiri sana sisi wakaazi wa Lamu ambao tumetegemea uvuvi kama kitega uchumi wetu watuondolee marufuku ya kutotoka nje ili tuwezekuvua samaki hata nyakati za usiku tuwezakujisaidia," alisema Mbwana.

Naye Mwenyekiti wa muungano wa wavuvi eneo la Faza Yusuf Athman ameitaka serikali kusitisha biashara za moja kwa moja na taifa la Somali ili kuwawezesha wavuvi hao kuendeleza biashara hayo kikamilifi na kuepukana na chanamoto za kiuchumi

Wakati uo huo, Mkurugenzi mkuu wa Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu Hassan Abdille ameitaka serikali kuu na ile ya kaunti ya Lamu kuhakikisha kuwa wanalijadili swala hilo na kuondoa marufuko hiyo ili kuwawezesha wakaazi wa Lamu kuimarisha uchumi.