Wawakilishi wa wadi katika Kaunti ya Mombasa wamewasilisha ombi kwa bunge la kaunti hiyo kutaka kupelekwa katika nchi jirani ya Tanzania ili kujifunza mfumo wa kuongoza kutoka kwa rais wa nchi hiyo John Magufuli.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza siku ya Ijumaa afsini mwake, Mwakilishi wa Wadi ya Tononoka Fahada Ahmed alisema kuwa rais huyo ameonyesha njia nzuri ya uongozi na wawakilishi wadi wametaka kujifunza kutoka kwake kuhusu mfumo wake wa uongozi.

“Katika siasa na uongozi kwa jumla, mtu hujikuza kutokana kwa kusoma kwa wengine ambao wako katika hadhi ya juu. Kwa kuwa Rais Magufuli ameonyesha uongozi mzuri, sisi tunaomba kupelekwa huko ili kujifunza kutoka kwake,” alisema mwakilishi wadi huyo.

Baadhi ya viongozi wamekuwa wakimpongeza Rais Magufuli kwa kupunguza ufisadi na utumizi mbaya wa fedha katika nchi ya Tanzania.