Wawakilishi wa bunge la kaunti ya Nyamira wamepanga kuandamana siku ya Alhamisi hadi kwenye ofisi ya kamishna wa kaunti hiyo Josphine Onung'a kulalamikia utendakazi wake. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kulingana na kiongozi wa walio wengi kwenye bunge la kaunti hiyo Laban Masira, ni kuwa ni jambo la kuhuzunisha kwamba wakazi wa kaunti wanaweza chinjwa tukiangalia. 

"Iweje kwamba watu wetu wanaweza angamizwa na majambazi ilhali kuna serikali inayostahili kuwahakikishia usalama na pia kulinda mali yao," aliuliza Masira.

Masira aliongeza kusema kuwa itawabidi wawakilishi wadi katika kaunti hiyo waandamane hadi kwenye ofisi za kamishna wa kaunti hiyo ili kulalamikia usalama wa wananchi.

"Kamishna wa sasa Josphine Onunga amefeli pakubwa serikali ya kaunti hii kuhusiana na hali ya kutuhakikishia usalama, na ndio sababu tumeamua kuandamana kesho hadi ofisini mwake kama njia mojawapo yakudhihirisha ghadhabu zetu kwake," aliongezea Masira.