Kwa mara nyingine tena wafuasi wa muungano wa Cord wameshiriki maandamano ya amani katikati mwa mji wa Nyamira kushinikiza kuondoka kwa makamishnna wa IEBC ofisini. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kulingana na mwekahazina wa chama cha ODM katika kaunti ya Nyamira ambaye vilevile ni mwakilishi wa wadi ya Manga Peter Maroro, wafuasi wa muungano wa Cord wataendelea kuandamana hadi pale makamishna wa tume hiyo watakapoondoka afisini. 

"Leo hii tumejitokeza kuandamana kuonyesha mshikamano wetu wa kutaka makamishna wa IEBC kuondoka afisini, na hatutaacha kuandamana hadi pale makamishna hao watakapoondoka ofisini," alisema Maroro. 

Kwa upande wake kiongozi wa vijana kwenye chama cha ODM katika kaunti hiyo Denis Marube, aliwarahi wakazi wa kaunti hiyo kujitokeza kwa wingi ili kuishinikiza tume hiyo kuondoka afisini. 

"Mashirika mengi yamepoteza imani na tume ya IEBC, ishara wazi kwamba wakenya hawana imani kwa tume hiyo kusimamia uchaguzi mwakani, na ndio maana nawaomba wakazi wa kaunti kujiunga nasi kwenye maandamano haya," aliongeza Marube.