Wakilishi wa wadi katika gatuzi la Mombasa wakiongozwa na mwakilishi wa wadi ya Tudor Patric Siminyu wameanzisha kampeni ya kumngo’a mamalkani spika wa bunge Thadius Rajwayi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Haya yanajiri siku chache tu baada ya kufanikiwa kumuondoa mamlakani aliyekuwa kiongozi wa wengi katika bunge hilo Abdallah Kasagamba. 

Inadaiwa kuwa zaidi ya wakilishi 14 tayari wameunga mkono hatua hiyo ambayo mapema mwezi Mei ililetwa mezani na mwakilishi mteule Bw. Mohamemed Hatimy. 

Karani katika bunge hilo Salim Juma alithibitisha kupokea mswaada uliyokuwa umetiwa sahihi na zaidi ya wakilishi 14 ukitaka kuondolewa madarakani spika wa bunge.

Spika wa bunge hilo Thadius Rajwayi anadaiwa kujihusha na visa vya ufisadi huku baadhi ya wakilishi akiwemo mwakilishi wa wadi ya Kongowea akipinga madai hayo, na kusema kuwa ni uvumi na maneno yasiyokuwa na msingi. 

Aidha, Bw. Oduor anadai kuwa tofauti katika bunge hilo sasa zimegeuka na kuwa za kikabila, huku baadhi ya wakilishi wa wadi wakipania kumwondoa spika wa bunge kwa sababu anatoka jamii flani, na sio kujihusisha na ufisadi kama inavyodaiwa.

Mwwakilishi wa Tononoka Saad Faraj amemtaka naibu spika Mswabah Rashid kuchukua nafasi ya Bw. Thadius Rajwayi.

Kumekuwepo na Baadhi ya wakilishi wakilalamikia kuwepo kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaochangia taharuki na migogoro inayoshuhudiwa mara kwa mara katika bunge hilo.