Wanaume wawili wameshtakiwa katika mahakama ya Mombasa kwa madai ya wizi wa kimabavu.
Ali Bakari na Hamadi Mbaru, wanadaiwa kumuibiwa Hussein Yusuf simu, nguo na shilingi elfu tano pesa taslimu.
Aidha wanakabiliwa na shtaka la kumjeruhi mlalamishi huyo baada ya kutekeleza wizi huo.
Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Jumatatu kuwa washukiwa hao wanadaiwa kutekeleza kitendo hicho tarehe 16 mwezi Machi, katika eneo la Check point huko Likoni.
Washukiwa hao walikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Richard Odenyo.
Hakimu Odenyo aliagiza kesi hiyo kusikizwa tarehe 17 mwezi Mei.