Hali ya huzuni ilitanda siku ya Jumamosi asubuhi katika kijiji cha Bombeta, Lokesheni ya Girango kwenye Wilaya ya Masaba Kaskazini baada ya mchanga kuangukia kisha kuwafunika na kuwauwa watoto wawili waliokuwa wakichimba mchanga wa kuunda nyumba ya matope.

Share news tips with us here at Hivisasa

Watoto hao kwa kawaida wenyeji huwatumia kwa kuwachimbia na kuwaletea aina ya mchanga huo wanaotumia kwa uundaji wa nyumba za matope.

Shughuli za uchimbaji wa mchanga huo umekuwa ukiendelea hasa ikizingatiwa msimu huu wa mvua unaonyesha kwa sasa. Watano wa waliojeruhiwa walipelekwa katika zahanati ya Nyagancha huku miili ya wawili hao zikipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Gucha, Keroka.

Akiwa sio mwepesi wa kusimulia matukio yaliyokuwa, Tabitha Onsongo ambaye ni mmoja wa walioponyoka kifo hicho alisema kuwa hata yeye angeaga dunia walakin akakwepa ajali hio kwa hiari yake Mwenyezi Mungu, “Ningekufa pia mimi, tulienda kuchimbba mchanga huo na wakati nilitoka kuchukua jembe ndogo tutolee mchanga, kuangalia nyuma nikaona umewafunika wenzangu waliobaki mle ndani,” alimaka nusura huyo.

Aidha wakaazi wa eneo hilo walikilaumu kiwanda cha majani chai cha Nyankoba kwa kusababisha mkosi huo kwani ndicho kimekuwa kikichimba mchanga huo na kuacha shimo wazi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kiwanda hicho ambaye alifika katika eneo la mkasa huo aliwalaumu wenyeji kwa kuenda mahala hapo kisiri na kuondoa mchanga kinyume na ilani iliokuwa imetolewa hapo awali kuwa hamna mtu anafaa kuuchimba mchanga huo.