Watu wawili walip[oteza maisha yao papo hapo katika ajali iliyofanyika Ijumaa tarehe 23 Septemba Tawi katika barabara ya Mombasa-Lungalunga.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Ajali hiyo ilihusisha gari mbili aina ya matatu na lori.

Inasemekana kwamba lori lilikuwa linajaribu kupita matatu moja iliyokuwa inabeba abiria wakati lilipokutana ana kwa ana na matatu nyingine iliyokuwa inatoka mbele.

Akithibitisha kisa hicho, Kamishna wa kaunti ya Kwale bwana Kutswa Olaka alisema kwamba majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya Msambweni kupata matibabu.

Ameongeza kwamba watafanya operesheni ili kuhakikisha kwamba magari mabovu hayaruhusiwi barabarani.

Ni majuzi tu wakazi wa eneo hilo walipofunga barabara hiyo kulalamikia hali yake mbaya kwani ajali nyingi zimefanyika hapo na wengi kupoteza maisha.