Mahakama ya Mombasa imewahukumu wanaume wawili waliopatikana na kosa la kumbaka mtoto mwenye ulemavu kifungo cha miaka 15 gerezani.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Dzombo Bakari Kadenge mwenye miaka 32 na Noro Sammy Athuman mwenye miaka 35, walipatikana na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 16, mwenye ulemavu wa kuongea na kusikia, mnamo Mei 4, 2015, katika eneo la Likoni.

Siku ya Jumatau, hakimu mkuu mkaazi Irene Ruguru alikitaja kisa hicho kama cha kinyama na kuongeza kuwa idara ya mahakama haitalegeza kamba katika kuangamiza visa vya ubakaji.

“Ni kisa cha kusikitisha kwa watu wazima kama nyinyi kumbaka mtoto mwenye ulemavu. Mahakama kamwe haitakubali visa kama hivi kuendelea,” alisema Ruguru.

Aidha, alisisitiza kuwa kifungo hicho kitakuwa funzo kwa wengine wanao endeleza ubakaji kwa walemavu.

“Kifungo hichi kitakuwa funzo kwa wale wanaoendeleza ubakaji kwa watoto na walemavu nchini,” alisema Ruguru.

Wawili hao walipewa siku 14 kukata rufaa kupinga kifungo hicho.