Watu wawili walipata majeraha jumatano baada ya basi kugongana na gari la kibinafsi katika eneo la Migaa kwenye eneo hatari la Salgaa katika barabara kuu ya Nakuru-Eldoret.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Walioshuhudia ajali hiyo walisema watu hao wawili walikuwa kwenye gari hilo dogo walipata majeraha na kukimbizwa katika hospitali kuu ya mkoa ya Nakuru Level Five iliyo mjini Nakuru ambapo wanauguza majeraha.

OCPD wa Rongai Joseph Mwamburi alidhibitisha tukio hilo akisema dereva wa gari hilo dogo alikuwa akijaribu kupita lori wakati ambapo liligongana ana kwa ana na basi liilokuwa likielekea magharibi mwa nchi kutoka Nairobi katika ajali hiyo iliyotokea asubuhi.

Hata hivyo alisema hakuna abiria yeyote wa basi aliyejeruhiwa.

Ajali hiyo ilisababisha msongamano wa magari kwenye barabara hiyo kuu ambayo kwa kawaida huwa na shughuli nyingi.