Mwanamume mwenye umri wa makamo na kijana mmoja mwenye umri wa miaka minane wanaendelea walinusurika kifo baada ya kupigwa risasi na maafisa wa polisi walipokuwa wakikabilianana genge la wezi huko Kisauni hapa mjini Mombasa.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kitsao Katana na Rajab Mohamed walijipata kuathirika na makabiliano hayo huko Magodoroni eneo la Soko Mjinga ambako kunaaminika kuwa makazi ya wengi wa wahalifu wanaowatatiza wenyeji wa Kisauni.

Rajab ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi ya Kengeleni alipigwa risasi kwenye kifua alipokuwa akitembea kuelekea shuleni yeye pamoja na ndugu yake mdogo na kufikia alhamisi risasi hiyo ilikuwa bado iko ndani ya kifua chake naye Katana ambaye ni makanga wa matatu za Kisauni kelekea mjini Mombasa alipigwa risasi kwenye sehemu zake za siri.

Kulingana mama Khadija Swaleh anasema alikuwa anajitayarisha kwa staftahi baada ya kumsikia mwanawe akilia. Anasema alipomuona mwanawe amesheheni damu mwilini mwake alimchukua na kumkimbiza katika kliniki moja mtaani humo alipoamriwa kumpeleka katika hospitali kuu ya pwani.

Hata hivyo mkewa Katana pamoja na mamake Rajab waliwakimbiza wawili hao katika hospitali kuu ya ukanda wa pwani.

Mkuu wa polis eneo la Kisauni Richard Ngatia amesema uchunguzi ulikuwa umeanzishwa kubaini wahusika wakuu wa visa vya mara kwa mara katika eneo la soko mjinga.