Watu wawili wamelazwa katika Hospitali Kuu ya Mkoa iliyoko mjini Nakuru baada ya kufunikwa na udongo kutoka kwa jengo moja ambalo liliporomoka siku ya Alhamisi.
Jumba hilo lilikuwa likiendelea kujengwa katikati mwa mji wa Nakuru.
Jamaa hao wawili waliokolewa na uma huku wakiwa wamepoteza fahamu katika tukio hilo ambalo lilifanyika karibu na Ofisi za Serikali ya Kaunti ya Nakuru.
Ni tukio lililowapelekea wakaazi waliokuwa karibu na eneo hilo kusalia wakiwa na wasiwasi huku ikiarifiwa kuwa jamaa hao walikuwa miongoni mwa wafanyikazi 20 waliokuwa wamepewa kibarua cha ujenzi wa jengo hilo ambapo walinusurika kifo.
Inadawai kwamba udongo ulio karibu na jengo hilo sio dhabiti, hatua ambalo ilichangia katika kuporiomoka kwa jengo hilo.
Naibu OCPD wa Nakuru Janet Wasike alidhibitisha tukio hilo akiarifu wanahabari kwamba ushirikiano baina ya maafisa wa polisi sawa na maafisa kutoka kwa shirika la Msalaba Mwekundu ulipelekea wawili hao kuokolewa na kukikmbizwa hospitalini.
Izingatiwe kuwa visa vya majengo kuporomoka viliripotiwa katika meneo mbalimbali kama vile mtaa wa Huruma jijini Nairobi mwaka jana na kupelekea baadhi ya watu kuuwawa.