Mwakilishi wa wadi ya Kiamokama iliyoko katika eneo bunge la Nyaribari Masaba, Kennedy Mainya amewapa changamoto wanafunzi kutia bidii masomoni ili wajisaidie katika siku zijazo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwakilishi huyo pia amewaomba wazazi kutuma maombi ya fedha za ustawi wa wadi ili kuwasaidia watoto wao kuendelea na masomo.

Akizungumza siku ya Jumatatu katika shule ya upili ya Mobamba ilyoko wadi yake katika hafla ya kepeana zawadi kwa wanafunzi waliofanya vyema katika mtihani wa kitaifa wa mwaka jana, Mainya alisema wengi wa wale wanaofaa kutuma maombi ya usaidizi wa fedha hizo hawakutuma na kuwaomba kutuma ili wanao waweze kunufaika na mpango huo wa serikali ya kaunti ya Kisii.

“Ninawaomba wazazi kutuma maombi ya pesa za Ward Development Fund kwa watoto wao ili waweze kupata pesa hizo za kugharamia masomo yao. Aidha, changamoto kuu tunayokumbana nayo ni kuwa wanaojiweza ndio wanatuma maombi ilihali mpango huu unkusudia kuwafadhili wasiojiweza katika jamii,” alisema Mainya.

Kwa upande wake, gavana wa kaunti ya Kisii, James Ongwae ambaye pia alihudhuria hafla hiyo ya kupeana zawadi, aliwaomba wazazi wa Kisii kukumbatia mpango huo kwani unalenga kuhakikisha wanafunzi kutoka familia maskini wanaendelea na masomo.

Gavana Ongwae aliahidi kuongeza fedha hizo kutoka milioni tatu mwaka huu wa matumizi hadi milioni tano katika bajeti ya mwaka ujao, ili kuwasaidia wanafunzi wengi wanaoonekana kuwa na mahitaji ya usaidizi.