Wazazi wameshauriwa kutilia mkazo swala la elimu ili kuboresha viwango cha elimu katika Kaunti ya Mombasa.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza afisini mwake siku ya Jumanne, afisa wa elimu katika gatuzi dogo la Likoni Salim Benerd, alisema kutozingatiwa kwa swala la elimu na wazazi kumechangia pakubwa watoto kukosa motisha wa kusoma.

Aidha, amedokeza kuwa kielelezo katika swala la elimu ni muhimu zaidi ili mtoto aweze kujitahidi kimasomo.

Afisa huyo amewasihi wazazi kuwa makini ili watoto wajiepusha na swala la anasa alilolitaja kuchangia pakubwa katika watoto kuacha shule.

Kwa upande wake, Fatma Mbarak, ambaye ni mwanasaikolojia, alisema kuwa jamii imehusika pakubwa katika kumvunja moyo mtoto katika swala la elimu, sambamba na wazazi kushindwa kudhibiti anasa kwa mtoto.