Wazazi jijini Mombasa wanapinga kubadilishwa kwa mfumo wa elimu ya 8-4-4 kwa kusema kuwa kubadilishwa kwa mfumo huo kutawatatiza wanafunzi.
Wakizungumza na mwanahabari huyu siku ya Jumatatu, Fatma Husein, mzazi wa watoto watatu, kutoka Nyali, alisema kuwa kubadilshwa kwa mfumo huo hadi ule wa 2-6-3-3-3 kutawafanya wanafunzi kuchangaanyikiwa ikizingatiwa wamezoea mfumo wa 8-4-4.
Hii ni ikiwa ya wataalam wa maswala ya elimu watakaokutana jijini Nairobi siku ya Jumatano ijayo, watafaulu katika majadiliano ya kuanza kwa mtaala mpya.
Zaidi ya wajumbe 500 wakiwemo wataalam wa maendeleo ya mtaala wa elimu wa kitaifa na kimataifa wanatarajiwa kukabidhiwa pendekezo la mtaala mpya kutoka kwa taasisi ya maendeleo ya mtaala KICD iliyokua ikifanya utafiti wa mpango wa elimu kuanzia mwaka jana.
Inakumbukwa kuwa waziri wa elimu Fred Matiang’ alipokutana na wanahabari jijini Nairobi alidokeza juu ya uwezekano wa kubadilishwa kwa mfumo wa 8-4-4.
Mojawapo ya mfumo utakaojadiliwa ni ule wa 2-6-3-3-3 ambao umetajwa kuhakikishia wanafunzi kupata uhodari na ujuzi wa kuafikia ruwaza ya 2030.
Naibu wa rais Willium Ruto natarajiwa kufungua rasmi kongamano hilo.