Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Christ the King Nakuru Niseta Munyi ametoa wito kwa wazazi kushirikiana na walimu kwa ufanisi.

Akizungumza wakati wa kusherehekea matokeo bora shuleni humo, Munyi alisema la muhimu ni ushirikiano baina ya wanafunzi, walimu na wazazi.

"Ufanisi ni wajibu wa kila mmoja wala si walimu pekee, tushirikiane sote na tutafaulu kama shule na jamii kwa jumla," alisema sister Munyi. 

Aliongeza kusema kuwa kando na shule hiyo kutoa mwanafunzi bora wa kike KCPE mwaka 2015, kibarua wanacho kuhakikisha matokeo bora hata zaidi katika miaka zijazo.

Wakati huo huo, mwalimu huyo amewataka wazazi kuzingatia maadili mema ya watoto wao na kuhakikisha wanapata elimu bora. 

"Wazazi wanafaa kuhakikisha watoto wao wanapata elimu bora ya maadili," aliongeza Munyi. 

Shule hiyo ya msingi ya Christ the king ilifanya vyema katika mtihani wa mwaka jana, huku mwanafunzi wa kwanza; Stacey Kemboi akipata alama 440.