Katika juhudi za kupambana na utumizi wa mihadarati katika kaunti ya Mombasa, wazazi na jamii kwa jumla wamehimizwa kuwajibikia majukumu yao vyema ili kuwalinda watoto wao kujitosa katika mihadarati.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea na mwanahabari huyu mjini Mombasa siku ya Jumatano, Naibu Kamishna wa kaunti ya Mahmoud Salim amesema kuwa lazima wazazi kuchukua jukumu la kufuatilia mienendo ya watoto wao na kuwalinda kujiunga na utumizi wa mihadarati.

Mahmoud amesema kuwa janga la mihadarati lisipokabiliwa mapema basi kwa kiasi kikubwa litaathiri kizazi kijacho kwani waathiriwa wengi kwa sasa ni vijana hali ambayo imechangia ukosefu wa usalama katika kaunti hiyo.

"Tunawaomba wazazi na jamii kwa jumla kuhakikisha kuwa inawalinda watoto wao pamoja na kuwashauri athiri za kutumia mihadarati ili tuwezekulinda kizazi chetu na kuwawezesha kutimiza ndoto zao katika siku za usoni," alisema Salim.

Salim ameshinikiza kuwepo na ushirikiano mwema baina ya jamii na maafisa wa usalama ili kukabili jinamizi hilo huku akiyataka mashirika ya kijamii kuhakikisha kuwa yanawahamasisha vijana kuhusu kujitenga na utumizi wa kihadarati.