Wazazi wote wa kaunti za Kisii na Nyamira wameulizwa kuwa na uwazi na kuwafunza wanao bila kuwaficha na kuwaelezea peupe watoto wao juu ya ugonjwa hatari wa ukimwi ili kulaizishia walimu kazi wakati wanapowasomesha watoto hao juu ya ugonjwa shuleni.
Akiongea ofisini mwake mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Daraja Mbili Flora Osusu amesema walimu huwa na wakati mgumu hasa wanapowafunza watoto hao.
“Wazazi wangekuwa na uwazi nakuwaelezea watoto wao juu ya ugonjwa wa ukimwi wangekuwa wanafahamu vyema nasi kama walimu kazi ingekuwa rahisi kuwaeleza saidi,”alielezea Osusu.
Aidha, amesema wazazi wengi wanapowaambia wanao usema hiyo ni njia ya aibu kwa watoto wao jambo ambalo ni kinyume na kisasi cha kaline ya ishilini na moja.Ameipongeza kanisa ya kikathoriki kwa kujitolea na kuja katika shule hiyo na kutoa mafunzo mahalumu kwa wanafunzi ambao limeleta mabadiliko kubwa kwa wanafunzi hao.
Kwingineko shule ya Daraja Mbili iko karibu na soko kuu la Daraja Mbili ilioko katika mji wa kisii, wanafunzi wengi hutoroka shuleni hasa siku ya Jumatatu na Alhamisi na kuenda kufanya biashara katika soko hilo .Osusu alisema wavulana hutoroka na kubeba mzigo katika soko hilo ili kujipatia riziki yao, kwa upande mwingine wasichana wa shule hiyo nao wanaenda kuokota matunda yale hutupwa na wanabiashara na kuyaosha na kuuza
Madamu Osusu amewaruhsu wanabiashara kuwa wakiwaona wanafunzi hao wakifanya kitendo hicho walipotiwe kwa afisi Kitu kinachosababisha haya nikutokana na hali mbaya ya maisha, wakati wengi wao wanatoka katika familia maskini.
Wanafunzi wa aina hiyo wanaposhikwa na kurejeshwa shuleni husema ni njaa inafanya kutekeleza kitendo hicho ,”alielezea mwalimu mkuu
Mwalimu huyo amesema shule zote zinastahili kuwa na orodha ya kuwalisha [feeding programs] wanafunzi ndani ya shule ili kuzuia kuchelewa kwa wanafunzi hao kwa masomo ya mchana na mwalimu huyo aliongezea kuwa kuna baadhi ya wanafunzi hurudi shuleni wakiwa na njaa .