Wazazi wote wa kaunti  za Kisii na Nyamira wameulizwa kuwa na uwazi  na kuwafunza wanao  bila kuwaficha na  kuwaelezea peupe watoto wao juu ya ugonjwa  hatari wa ukimwi ili kulaizishia walimu kazi wakati wanapowasomesha watoto hao juu ya ugonjwa shuleni.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea  ofisini mwake mwalimu mkuu wa shule  ya msingi ya Daraja Mbili Flora  Osusu amesema walimu huwa na wakati mgumu hasa wanapowafunza watoto hao.

“Wazazi wangekuwa na uwazi nakuwaelezea  watoto wao  juu ya ugonjwa wa ukimwi wangekuwa wanafahamu vyema nasi kama walimu kazi ingekuwa rahisi kuwaeleza saidi,”alielezea Osusu.

Aidha, amesema  wazazi wengi wanapowaambia wanao usema hiyo ni njia ya aibu kwa watoto wao jambo ambalo ni kinyume na kisasi cha kaline  ya ishilini na moja.Ameipongeza kanisa ya kikathoriki kwa kujitolea na kuja katika shule hiyo na kutoa mafunzo mahalumu kwa wanafunzi ambao limeleta mabadiliko kubwa kwa wanafunzi hao.

Kwingineko shule ya Daraja Mbili iko karibu na soko kuu la Daraja Mbili ilioko katika mji wa kisii,  wanafunzi wengi hutoroka shuleni hasa siku ya Jumatatu na Alhamisi  na kuenda kufanya biashara katika soko hilo .Osusu alisema wavulana  hutoroka  na kubeba mzigo katika soko hilo  ili kujipatia riziki yao, kwa upande mwingine wasichana wa shule hiyo nao wanaenda kuokota matunda yale hutupwa na wanabiashara na kuyaosha na kuuza

Madamu Osusu amewaruhsu wanabiashara  kuwa wakiwaona wanafunzi hao wakifanya kitendo hicho walipotiwe kwa afisi Kitu kinachosababisha haya nikutokana na hali mbaya ya maisha, wakati wengi wao wanatoka katika familia maskini. 

Wanafunzi wa aina hiyo wanaposhikwa na kurejeshwa shuleni husema ni njaa inafanya kutekeleza  kitendo hicho ,”alielezea mwalimu mkuu

Mwalimu huyo amesema shule zote zinastahili kuwa  na orodha ya kuwalisha [feeding programs] wanafunzi ndani ya shule ili kuzuia kuchelewa kwa wanafunzi hao kwa masomo ya  mchana na   mwalimu huyo aliongezea kuwa kuna baadhi ya wanafunzi hurudi shuleni wakiwa  na njaa .