Wazazi wote katika kaunti ya Kisii wameshauriwa kuripoti katika afisi ya mkurugenzi wa elimu katika kaunti hiyo ikiwa kuna shule inaendeleza mafunzo ya ziada wakati wa likizo ili shule hiyo ichukuliwe hatua kali za kisheria.
Ushauri huo umetolewa baada ya kubainika kuwa kuna baadhi ya shule ambazo huendesha masomo ya ziada wakati shule zimefungwa jambo ambalo ni kinyume na sheria.
Akizungumza afisini mwake mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Kisii Richard Chepkawai aliwashauri wazazi kuripoti ikiwa kuna shule inaendesha masomo wakati wa likizo ili kujilimbikizia pesa ambazo hazijulikani na serikali.
“Serikali ya kitaifa ilifutilia mbali masomo ya ziada wakati wa likizo na ninaomba wazazi kutupa ripoti ikiwa kuna shule inakiuka sheria hiyo,” alisema Chepkawai.