Share news tips with us here at Hivisasa

Shule ya msingi ya Umoja Lanet, iliyoko katika eneo la Nakuru Kaskazini, imeagiza kila mtoto anayejiunga na shule hiyo kununua dawati lake.

Akizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumatano, mwalimu mkuu katika shule hiyo, Cyrus Mugi, alisema kuwa ni jambo ambalo wazazi na viongozi wanaosimamia shule hiyo walikubaliana nalo.

“Baada ya wazazi kununa madawati hayo, shule hii huchukua jukumu la kuyatunza hadi pale watoto watakapokamilisha darasa la nane,” alisema Mugi.

Hata hivyo, mwalimu huyo mkuu alisema kuwa wanafunzi hao huwa hawarudi nyumbani na dawati hizo wanapomaliza darasa la nane.

Alidokeza kwamba madawati hayo hutumika katika kubadilisha yale ambayo yamevunjika na mengine hupatiwa watoto wasiyojiweza haswa mayatima.

Mugi laisema kuwa shule hiyo huwapa mayatima nafasi ya kusoma bila kulipa karo.

Baadhi ya wazazi katika shule hiyo waliozungumza na mwandishi huyu walisema kuwa jambo hilo la kujinunulia dawati ni nzuri, kwa kuwa linawapa muda wa kujipanga kwa kulipa viwango vidogo vya fedha hadi malipo ya kupata madawati hayo yanapokamilika.