Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wazazi wameonywa dhidi ya kuwatelekeza wanao na badala yake wanafaa kushirikiana na walimu katika kukuza maadili.

Wito huo umetolewa na mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Crater mjini Nakuru Esther Okuto.

Akizungumza shuleni humo siku ya Ijumaa wakati wa hafla ya shukrani kwa matokeo bora, Okuto alisema kwamba ni jambo la kusikitisha kwa wazazi kuwatelekeza watoto.

"Wazazi mnafaa kushirikiana na walimu kukuza maadili ya wanafunzi na si kuwaachia tu walimu" Okuto alisema.

Hata hivyo ameshukuru wote walioshirikiana mwaka jana kuhakikisha matokeo mema ya KCPE.

Shule hiyo iliandikisha matokeo bora ikilinganishwa na mwaka wa 2014.