Jamii imetakiwa kujizatiti katika kukabiliana na swala la mimba na ndoa za mapema katika eneo la Pwani.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wazazi wametakiwa kukoma kusingizia umaskini kama sababu kuu ya mimba na ndoa za mapema, na badala yake kuwa mstari wa mbele kukabiliana na janga hilo.

Akizungumza siku ya Jumatatu, mwanasaikolojia Fatma Mbarak, alisema jamii imeshindwa kutambua shida zinazowakabili watoto, hasa wakike, kutokana na wazazi kutafuta mbinu za kujikimu kimaisha.

Mbarak alisema kuwa hali hiyo inachangia wasichana wengi kuathirika kifikra kutokana na kukosa watu wa kuwaelekeza kimaadili.

“Ukosefu wa wazazi kutimiza majukumu yao ya kinyumbani sambamba na migogoro ya kifamilia pia imechangia pakubwa mimba za mapema katika jamii,” alisema Mbarak.

Vile vile ameeleza kuwa kuna haja ya jamii kuelimishwa kuhusu jinsi ya kuwalea watoto wao ili kuwaepusha na majanga kama hayo.