Wazazi katika ukanda wa Pwani wametakiwa kutosuluhusha kesi za dhuluma dhidi ya watoto nyumbani na badala yake kuachia Idara ya Mahakama kutekeleza wajibu wake.
Kauli hii inajiri baada ya visa vya dhuluma dhidi ya watoto kuripotiwa kuongezeka katika eneo la Pwani.
Kwenye mahojiano ya kipekee na mwandishu huyu siku ya Jumatano, afisa wa maswala ya kijinsia katika Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika Salma Hemed, alisema wazazi hushawishiwa kuzisuluhisha kesi hizo nje ya mahakama, hali inayomuacha mtoto na mateso mengi ya kisaikolojia.
Hemed alisisitiza kuwa ni sharti jamii ya Pwani kuhakikisha kwamba inachukua jukumu la kuripoti tukio lolote lile la dhuluma dhidi ya mtoto, ili dhuluma hizo zikomeshwe kupitia mkono wa sheria.
“Ningependa kuwahimiza wazazi kuhakikisha kwamba wanatekeleza majukumu yao kikamilifu katika kuzilinda haki za watoto wao,” alisema Hemed.