Wazazi wa shule ya Heroes High School walivamia shule ya Kirobon kwa magari matatu ya utumishi wa umma, ambapo mwalimu mkuu, Hilda Muriuki, alihamishiwa mwanzoni mwa muhula na kudai kuwa uhamisho huo uondolewe.
Wazazi hao waliokua na hasira hata hivyo, walinyimwa haki ya kuingia na walinzi katika shule na kusababisha mwalimu mkuu kutembea hadi mlango na kuongea nao.
Alipojaribu kuwaongelesha alibebwa juu juu na kuingizwa kwa gari iliyompeleka hadi shule ya Heroes.
Alikaribishwa kwa nyimbo na nderemo.
Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri waliotembelea shule hiyo pamoja na mjumbe na maafisa wa elimu kutoka ofisi ndogo ya kata alitoa wito kwa wazazi kuruhusu idara ya elimu kushughulikia hali hiyo.
Alisema kuwa alishauriana na waziri wa elimu Fred Matiang'i ambaye alikuwa ameleekeza uhamisho huo utupiliwe mbali.
Alisema kuwa Muriuki atarejea tena ofisi mara baada ya barua rasmi kufika kama ilivyoagizwa na waziri.